Huyu mdada Elizabeth Lambert alikuwa akiichezea soka timu yake ya Chuo Kikuu cha New Mexico lakini kwa sasa amesimamishwa pasipo muda maalumu kuichezea timu hiyo kutokana na visa vyake vya kupiga na kukwatua kwa makusudi ya kuwaumiza wachezaji wa timu pinzani. Amekuwa akifanya hivi kwa muda na akawa anaachiwa ama kupewa onyo la kadi ya njano tu, hata kumkwatua mtu kwa nyuma au kumpiga ngumi anaishia kupewa tu kadi ya njano badala ya nyekundu na pengine faini na onyo kali. Baadhi ya video hizi inaonesha kuwa wakati mwingine amefanya vitendo hivi kama kinga binafsi pale anapoguswa ama kubughudhiwa, kwenye video hiyo hapo chini utaona dada mmoja akimpiga kipepsi cha tumbo na mwingine akiikamata bukta yake, yeye majibu yake ni kuwakwida. Ukomo wa haya yote umefika baada ya video kupostiwa katika mtandao jamii wa video, YouTube, juu ya tukio la Elizabeth kumfanyia vitimbi mchezaji wa timu ya Chuo Kikuu cha Bringham Young. Hati posti hii inawekwa hewani, video hiyo imeshapata utazamaji mara 3,321,459. Isingekuwa ni video hiyo kuwekwa hadharani, mdada huyu angeendelea tu kutesa kiwanjani kama ambavyo alikuwa akitesa kabla ya hapo. Tizama video hapo chini toka youtube.com/yMao8hDtnxk